Ticker

7/recent/ticker-posts

SIMBA YAKIRI NGOMA NZITO MOROKO ,YAAHIDI KUPAMBANA

MENEJA Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Ahmed Ally amesema wana mlima mrefu wa kupanda nchini Moroko dhidi ya klabu ya Wydad Casablanka, lakini wanajiandaa ili kufanya vizuri.

Ahmed alisema ni lazima wakiri kuwa wamepata mpinzani mgumu kwenye hatua ya Robo fainali na pengine ni mpinzani mgumu zaidi tangu waanze kushiriki hatua hii.

"Hapa unamzungumzia bingwa mtetezi, unamzungumzia mshiriki wa Club world Cup, unazungumzia timu yenye wachezaji waliotoka nusu fainali ya kombe la dunia

"Huu ni mlima mrefu kwetu lakini hatuna budi kuupanda na kufika kileleni


"Ili uwe mkubwa Afrika ni lazima uwafunge wakubwa wa bara hili

"awezekana sana Simba kupata ushindi dhidi ya Wydad kama tuu kila idara ndani ya taasisi yetu itatimiza wajibu wake kwa asilimia 100

"Kama tulivyomvua ubingwa Zamalek mwaka 2003 ni wakati sasa kumvua Ubingwa Wydad." amesema Ahmed.

Post a Comment

0 Comments