Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi ametunukiwa Tuzo maalumu ijulikanayo kama VIP Global Water Changemakers Awards kutokana na jitihada zake za kuifanya Zanzibar kuwa nchi ya kwanza barani Afrika kuanzisha na kuzindua programu ya uwekezaji katika sekta ya maji.
Tuzo hiyo imetolewa wakati wa mkutano wa maji wa Umoja wa Mataifa Machi 22,2023 jijini New York, Marekani.
Rais Dkt. Mwinyi atakabidhiwa rasmi kesho tuzo hiyo ya Kimataifa ya Mabadiliko ya Sekta ya Maji.
0 Comments