Mhe. Mhagama kulia pamoja na Mhe. Simbachawene, wakila kiapo Ikulu leo.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan leo amewaapisha mawaziri wawili aliowafanyia mabadiliko ya wizara jana, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mawaziri hao ni Jenista Joakim Mhagama aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).
Mhagama ambaye awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, anachukua nafasi ya George Boniface Simbachawene ambaye nae ameapishwa leo.
Simbachawene ameteuliwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menijimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, akichukuwa nafasi ya Mhagama.
0 Comments