Ticker

7/recent/ticker-posts

LISSU AREJEA NCHINI NA KUANZA NA RIPOTI YA CAG

Makamu Mwenyekiti wa Chadema Tundu Lissu 

Tundu Lissu amerejea Tanzania kutoka Ubelgiji anakoishi kwa muda mrefu sasa.

Kiongozi wa upinzani nchini amerejea mapema leo na moja kwa moja kuzungumzia suala la ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Akihojiwa mara baada ya kutua nchini, Lissu alisema hakuna kipya kwenye wizi huo zaidi anaamini umeongezeka.

"Hakuna kipya, wizi ni uleule, wezi ni walewale, Chama ni kilekile na viongozi ni walewale, hili sio jambo jipya."

Akizungumzia kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutama wezi wampishe.

Lissu alisema Rais ndie mwajiri Mkuu hivyo anaouamuzi wa kuchukua Kwa mtu yeyote bila kumuomba.

Hii ni mara ya pili kwa mwaka huu kwa Lissu kurejea  Tanzania, alifanya hivyo Januari 23  na kile alichokitaja kuwa "kuandika ukurasa mpya" katika safari yake ya kisiasa.


Lissu aliyepigwa risasi mara 16 katika tukio la kujaribu kumuua mwaka 2017 na kuishi uhamishoni Ubelgiji tangu wakati huo.

Kiongozi huyo wa upinzani aliye na miaka 55 amerejea nchini huku akisita kusema kama amerejea moja kwa moja ama ataondoka tena.

"Si mlisema sitarudi na kwamba nimekimbia...haya ya kurudi au kutorudi moja kwa moja tutalizungumza..."

Awali Lissu alitangaza uamuzi wake wa kurejea nyumbani baada ya Rais Dkt. Samia kuondoa marufuku ya mikutano ya kisiasa  iliyokuwa imewekwa na mtangulizi wake hayati John Magufuli.

Post a Comment

0 Comments