Ticker

7/recent/ticker-posts

JANUARY MAKAMBA KISIKI KISICHOOZA

NIKIWA MKUBWA NATAKA KUWA KAMA JANUARY MAKAMBA

Na Mfalme Huihui

Mitandaoni anapigwa mawe kila aina. Yeye hajibu. Yupo kimya. Very serious na kazi. Leo unapokea taarifa kuwa vigogo wanne kutoka Wizara yake ya Nishati, wametemeshwa mzigo kwa ufisadi.

Soma jina. January Makamba. Waziri wa Nishati. Umewahi kumwona anabishana au kuraruana mitandaoni? Ngozi ngumu sana. Mwanaume sana.

Meneja Mkuu wa TanOil, Kapuulya Musomba. Meneja wa Fedha na Utawala, James Batamuzi. Meneja Hifadhi wa Mafuta, Sudi Abdallah. Meneja wa Usambazaji na Uendeshaji, Amour Marine. Wote wapigwa chini.

Sababu ni kubainika ubadhirifu kwenye Shirika la TanOil, ambalo lipo ndani ya Wizara ya Nishati. Waziri ni January. Baada ya kusoma ripoti iliyoonesha madudu, wahusika wamepigwa chini.

Soma kauli ya January... “Tulifanya ukaguzi baada ya kubaini wanatudanganya. Hatutaishia TanOil. Tutafanya ukaguzi wa uendeshaji wa kila taasisi ya wizara na kuchukua hatua za haraka.”

Yaani, wakati watu wanashinda na kukesha mitandaoni kumpakaza shombo, yeye yupo busy na kazi. Hasubiri ripoti za CAG. Anaagiza ukaguzi wa ndani na kuchukua hatua.


Ungedhani mitandao itamwondolea focus. Hata kidogo. Yupo focused na majukumu ya kujenga nchi. Na mafisadi wizarani wanamkoma.

Kipindi cha uongozi wa jiwe, alitafutwa kila mahali ili atumbuliwe. Jiwe akamkosa. Wakaamua kumtega. Wakamrekodi akiongea na baba yake.

Kipindi cha jiwe, hukumwona popote akitoa mapambio. Yeye mpe kazi, afanye. Ukimpa uwaziri anakuwa waziri. Hawi chawa wa Rais. Hakuwa chawa wa Jiwe.

Kipi hajasemwa? Ufisadi? Alishatupiwa kila uchafu. Jiwe akiwa Rais, akampekua kila mahali hakukuta kitu. Hakujipendekeza. Alibaki imara. Unadhani alivyomdindia Jiwe, kama angekuwa fisadi, angemwacha?

Mimi nikiwa mkubwa nataka kuwa kama January. Mambo yanakuja na kupita ila hayamwondoi kwenye mstari. Soma jina, January Makamba.

Imeandikwa na: 

Mfalme Huihui,

Nyegezi, Mwanza.

Post a Comment

0 Comments