Ticker

7/recent/ticker-posts

WAFUKUA KABURI NA KUKATA SEHEMU ZA SIRI ZA MAITI

KATIKA hali ya kustaajabisha na kushangaza, watu wasiojulikana wamefukua kaburi lililokuwa limezika mwili wa Ruben Kasala (74) kisha wakakata sehemu za siri za marehemu na kuondoka nazo.

 

Tukio hilo limetokea katika Kijiji cha Kasokola Kata ya kasokola Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi, jioni ya Machi 18,2023. Aliyethibitisha tukio hilo ni mtoto wa marehemu, Frank Kasala.

 

Mtoto huyo wa marehemu amesema kilichomuua baba yao ni maradhi kwani kwa muda mrefu alikuwa akisumbuliwa na sukari na changamoto ya mapafu. Baba yake alifariki dunia Machi 18, 2023 na familia ilimzika siku hiyo hiyo.

 

 Alisema waligundua tukio hilo asubuhi ya Machi 18,2023 baada ya kwenda kuzuru kwenye kaburi hilo, ambapo walikuta kaburi limechimbwa na mwili wa baba yao umefukuliwa, sanduku limevunjwa kabisa,  wakatoa walichokitaka kisha wakarudisha na wakafukia kidogo na udongo.

 

Hata hivyo tunasubiri uchunguzi uchunguzi zaidi wa serikali ili kujua kilichofanyika na sababu ya kufanyika.

Post a Comment

0 Comments