Simon Msuva
BAADA ya timu za Tanzania ngazi ya klabu kuonesha ubabe kwenye michuano ya kimataifa inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF), Sasa ni zamu ya timu ya taifa, Taifa Stars kufanya kile kilichofanywa na Simba na Yanga.
Simba na Yanga kwa mara ya kwanza zote zimeingia hatua ya robo fainali ya michuno mikubwa miwili ya ngazi ya klabu inayoandaliwa na CAF.
Simba imeingia robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika na Yangabinawakilisha nchi kwenyebkombe la Shirikisho hatia ya Robo fainali, Taifa Stars nayo imeonesha dalili za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Uganda kwenye mchezo wa Kundi F leo uliochezwa kwenye uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri.
Simon Msuva anayechezea klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia ndio shujaa wa mchezo huo baada ya kufunga bao hilo katika dakika ya 68 ya mchezo akimalizia krosi ya beki wa Yanga, Dickson Job na kumpa mwanzo mzuri kocha Mualgeria, Adel Amrouche.
Ushindi huo unaifanya Taifa Stars ifikishe pointi nne na kusogea nafasi ya pili nyuma ya Algeria yenye pointi tisa, wakati Uganda ikisalia na pointi moja na kuburuza mkia nyuma ya Niger yenye pointi mbili baada ya timu zote kucheza mechi tatu.
Timu hizo zitarudiana Jumanne Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
0 Comments