Ticker

7/recent/ticker-posts

MUDA WA KUTOA HUDUMA ZA UMEME ZANZIBAR WABADILISHWA

 

KUELEKEA Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limetangaza mabadiliko ya muda  wa kutoa huduma kwa wakazi wa visiwa hivyo.

Mabadiliko hayo yatavigusa vituo vya kuuzia umeme (TUKUZA), ambapo vituo vya Mjini na Magharibi vitaanza kazi saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni na kwa muda wa usiku vitaanza kazi saa 1:30 hadi saa 4:00 usiku.

 Kwa wateja wa kawaida na wakubwa (KWILIAM) vituo vitaanza kazi saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.

 

Aidha vituo vya kuuzia umeme TUKUZA na huduma za kawaida  vya Makunduchi, Mkokotoni na Gamba vitaanza kazi saa 2:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.  

Post a Comment

0 Comments