Ticker

7/recent/ticker-posts

KOBE MKONGWE ALIYEZAA WATOTO 800 ASTAAFU

 

Diego katika muonekano tofauti

KOBE mkubwa na mkongwe aliyejizolea umaarufu kwenye maeneo mbalimbali duniani ameamua kustaafu kuzaa baada ya kufanikiwa kuzaa watoto 800 katika kipindi chote cha maisha yake.


 Kobe huyo ambaye anajulikana kwa jina la Diego kwa sasa ana umri wa miaka 103. Diego anatajwa kushiriki katika harakati za kuokoa kizazi chake kutoweka, ambapo inaelezwa asilimia 40 ya kobe 2,000 ambao sasa wanaishi kwenye kisiwa cha Española Diego ni wa kwake.


 Diego ana uzito wa 80kg, urefu 90cm na urefu wa 1.5 mita, alikuwa sehemu ya mpango wa kuzalisha kobe zaidi katika kisiwa cha Santa Cruz, kwa miongo kadhaa kabla ya kuachiliwa ili aishi siku zake zote katika kisiwa alichozaliwa, Española. 


 "Amechangia asilimia kubwa katika ukoo ambao tunarudisha Española.Kuna hisia ya furaha kuwa na uwezekano wa kumrudisha kobe huyo katika hali yake ya asili," alisema Jorge Carrion ambaye ni mkurugenzi mkuu wa hifadhi hiyo. 


 Diego alihifadhiwa kama njia ya kulinda mradi wa mazingira katika kisiwa hicho kidogo, Diego na kobe wengine ambao aliachiliwa nao, waliwekwa karantini, ili kuzuia kuhamisha mimea yoyote kutoka kisiwa kingine. 


 Inaaminika kwamba Diego alichukuliwa kutoka Galápagos karibu miaka 80 iliyopita na wanasayansi. Kisha alipelekwa San Diego Zoo katika jimbo la California kabla ya kuhamishwa hadi kisiwa cha Santa Cruz, miaka 50 iliyopita. 


Hapo ndipo alipowekwa kwenye mpango wa kuzaliana na kobe wengine 15. Walipochukuliwa mara ya kwanza, kulikuwa na kobe wawili wa kiume na 12 wa kike kutoka katika spishi za Diego. 


 Kobe wakubwa ndio walioishi kwa muda mrefu zaidi kati ya wanyama wote wenye uti wa mgongo kwa wastani wa zaidi ya miaka 100. Kobe wakubwa zaidi kwenye rekodi waliishi hadi miaka 152. 

Post a Comment

0 Comments