Ticker

7/recent/ticker-posts

APOTEZA MAISHA AKIFANYA MAPENZI KICHAKANI

 

WAPENZI wawili nchini Kenya wamejikuta wakitenganishwa na kifo baada ya mmoja kati yao kupoteza maisha wakati akiwa katikati ya mahaba.

Aliyepoteza maisha ni mwanamke aliyefahamika kwa jina moja la Milca mwenye umri wa miaka 48, imeelezwa kuwa mwanamke huyo alikuwa akifanya mapenzi na mwanaume anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake.


Wawili hao waliingia kichakani eneo la Mbita kaunti ya Homa Bay kwa lengo la kufanya mapenzi huku wakiwa wamelewa. Mwanaume aliyekuwa na Milca anadaiwa kuwa na miaka 37 na tayari anakabiliwa na mashtaka ya mauaji.


Tukio hilo limetokea jioni ya Jumapili ya Machi 19 mwaka huu baada ya wapenzi hao waliokuwa wanarejea nyumbani kuamua kuingia kwenye kichaka eneo la Got Rateng kwa ajili ya kufanya kitendo hicho walipokuwa wametoka kunywa pombe, tovuti ya TUKO imeripoti.

 

Chifu wa eneo hilo amesema kuwa wawili hao  awali walikuwa wameonywa wasishiriki tendo wakiwa wamelewa lakini hawakutii, mshtakiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo baada ya kukiri chanzo cha kifo hicho.

Post a Comment

0 Comments