Kipigo hicho kimetazamwa kama ni hasira kwa timu ya Simba yenye maskani yake mtaa wa Msimbazi, jijini Dar es salaam katika kuomboleza kifo cha kikatili kilichomkumba Simba wa Serengeti, dume la mbegu, mfalme wa mbuga maarufu kama Bob Junior aliyeuwawa na Watoto wake hive karibuni.
Chama akishangilia moda ya magoli yake kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika |
Chama aliweza kuwadhoofisha wapinzani wao kwa kutundika bao tatu kimiani katika dakika ya 10 kwa shuti kali la mpira wa adhabu, dakika ya 36 kwa penati na dakika ya 70, bao alilolifunga kwa utulivu mkubwa.
Aidha ameshiriki kwa kutoa pasi ya moja kwa moda au kuanzisha mashambulizi yaliyozaa mabao manne zaidi yaliyofungwa na mkongomani Jean Beleke dakika ya 32 na 65 na kiungo raia wa Mali Sadio Kanoute katika dakika ya 54 na 87.
Matokeo hayo yanaifanya Simba kuendelea kushika nafasi ya pili ya kundi C ikiwa na pointi tisa nyuma ya Raja Casablanka ya Moroko yenye pointi 13 ambayo leo imetoka sare ya 1-1 na Vipers ya Uganda.
Simba itamaliza mechi yake ya mwisho ya hat ya makundi Machi 31 dhidi ya Raja Casablanka, mchezo utakaochezwa nchini Moroko.
0 Comments