Ticker

7/recent/ticker-posts

JET YASISITIZA UTUNZAJI WA MISITU NCHINI

Mkurugenzi wa JET, John Chikomo

Katika kuadhimisha kilele cha siku ya misitu duniani, inayoadhimishwa Machi 21, ya kila mwaka, Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) kimetoa rai kwa watanzania kutokata miti hovyo Ili kulinda misitu yetu.

Mkurugenzi wa JET, John Chikomo ndie aliyetoa rai hiyo mapema leo.

Amesema misitu ni uhai, na uhai unapaswa kulindwa kwa gharama yeyote ile na Ili kulifanikisha hilo, Kila Mtanzania anapaswa kubeba jukumu la kutokata miti na badala yake tunatakiwa kuipanda zaidi.


JET inatoa pongezi kwa serikli na wadau wa Misitu kwa kuwa mstari wa mbele katika kuilinda.

Aidha JET inawashauri wanachama wake na Waandishi wa Habari kwa ujumla kuwa mstari wa mbele kupanda na kuhamasisha upandaji, ukuzaji na utunzaji wa miti ili kushiriki mapambano dhidi ya  changamoto  ya mabadiliko ya tabia nchi.

Post a Comment

0 Comments