Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi akiweka jiwe la msingi katika Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania(TAEC)-Zanzibar. |
NA MWANDISHI WETU, AFRINEWS ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Bodi na Menejimenti ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) kwa kuona umuhimu wa ujenzi wa Ofisi na maabara kwa lengo la kuimarisha huduma za Nguvu za Atomu Zanzibar.
Aidha, Dk. Mwinyi amesema Uwekezaji huu utaimarisha udhibiti wa matumizi salama ya mionzi pamoja na kuimarisha utafiti, ubunifu na matumizi ya sayansi na teknolojia ya nyuklia.
Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipoweka jiwe la msingi katika Ofisi na Maabara ya Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania(TAEC)-Zanzibar.
0 Comments