Ticker

7/recent/ticker-posts

MTUHUMIWA WA MAUAJI YA MKE WA MWENYEKITI KAGERA AKAMATWA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera ACP William Mwampagale 


 

NA MWANDISHI WETU, AFRINEWS KAGERA


NJAA haizuliki, hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera kufanikiwa kumdaka kiulaini Paschal Kaigwa Mariseli (21) ambaye anatuhumiwa  kwa mauaji ya mke wa Mwenyekiti wa Mtaa wa National Housing, kata ya Rwemishenye Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera Bi. Khadija Ismail (29). 


Mariseli ambaye ni mzaliwa wa Kijiji cha Katerero, Kata ya Kishogo, Wilaya ya Bukoba inadaiwa kabla ya kutekeleza ukatili huo alikuwa akiishi kwenye familia ya Mwenyekiti huyo.


Tangu alipotekeleza mauaji hayo jioni ya Februari 13,2023 baada ya kumpiga na ubao na kisha kumbaka, inadaiwa kuwa alikimbia na Jeshi la Polisi Mkoani Kagera kwa kushirikiana na Wananchi walikuwa wakimsaka hadi alipopatikana Februari 19,2023.


Akiongea na Waandishi wa Habari leo Februari 21, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani Kagera ACP William Mwampagale amesema mtuhumiwa huyo  kwa kipindi alichotoweka alikwenda kujficha vichakani, hata hivyo  Februari 19, 2023 majira ya saa 10 jioni alizidiwa na njaa na ndipo alipoamua kutoka ili kwenda kutafuta chakula.


Marehemu Khdija Ismail
Kamanda amesema mtuhumiwa alikwenda kutafuta msaada wa chakula nyumbani kwa shangazi yake kwenye mtaa wa Kashai  Manispaa ya Bukoba, hata hivyo akiwa njiani alikutana na watu waliomtambua na kuanza kupiga   Kelele na na kufanikiwa kumkamata.

 

Aidha Kamanda Mwampagale amewashukuru Wananchi wote Mkoani humo kuendelea kutoa ushirikiano wa kuwafichua  wahalifu.

 

Kamanda Mwampagale ametoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo mbali mbali vya uhalifu ikiwemo mauaji, ubakaji na ukatili  mkoani humo kuacha mara moja, kwani Messi la polisi liko imara na ameahidi kuwashughulikia kikamilifu.

Post a Comment

0 Comments