Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo ametengua uteuzi wa viongozi watano kama inavyoonekana kwenye taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Zuhura Yunus.
Viongozi hao ambao wameondolewa kwenye nafasi zao tangu Januari 22, 2023 ni Mkuu wa wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mara, Msongela Nitu Palela, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Singida, Michael Augostino Matomora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga, Linno Pius Mwegeni na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Njombe, Sunday Deogratius Ndori.
0 Comments