Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo
Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajiwa kuanza kufundishwa kwenye shule za Msingi na Sekondari nchi nzima.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo ndio wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais kuanzia Julai 2022 hadi Desemba 2022 kwenye Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria leo Januari 24, 2023 katika Ofisi za Bunge jijini Dodoma.
“Mheshimiwa Mwenyekiti, katika muendelezo wa utoaji wa elimu ya Muungano tumefuatilia Ithibati ya Kitabu cha Historia ya Muungano ili kiweze kutumika kama Kitabu cha ziada kwa shule za Msingi na Sekondari pia kutoa elimu ya Muungano mashuleni na katika vyuo vya elimu ya juu,” amesema.
Alisema katika kuhakikisha serikali inaendelea kutatua hoja za Muungano zilizosalia Dkt. Jafo amesema kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais inatarajia kuratibu Vikao vya Kamati ya Pamoja ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (SJMT) na SMZ vya kushughulikia masuala ya Muungano.
Aidha, Waziri Jafo ameongeza kuwa ili kuhakikisha utekelezaji unafanyika ipasavyo Serikali inatarajia kufanya ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa maagizo yaliyotolewa na Kamati ya Pamoja na yale masuala 22 ya Muungano kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa upande mwingine Dkt. Jafo amesema kuwa Serikali inatarajia kufanya ufuatiliaji wa utekelezaji wa programu na miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya pande mbili za Muungano ikiwa ni pamoja na kuratibu utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo kwa Majimbo ya Zanzibar.
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania |
Semina hiyo imelenga kuwaongezea makali wabunge hao katika usimamizi wa fedha za Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo kwa wabunge.
Aliweka wazi kuwa serikali pia imepanga kufanya ufuatiliaji wa gawio kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) pamoja utekelezaji wa Taasisi za Muungano katika kipindi hicho.
Kwa upande wake Makamu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria ameitaka Ofisi ya Makamu wa Rais kuendelea kutoa elimu kuhusu masuala ya Muungano ili wananchi wapate uelewa.
0 Comments