NA MWANDISHI WETU
Mwenyekiti wa chama cha Waandishi wa Habari za mazingira Tanzania (JET), Dkt. Ellen Otaru-Okoedion ameteuliwa kuziwakilisha Asasi za Kiraia za Afrika kwenye Kamati ya Utendaji ya Dunia ya Ushirikiano wa Kukabiliana na Ukame inayojulikana kama Riyadh Global Drought Partnership (RGDRP).
Dkt. Otaru ni Mhadhiri na mdau wa masuala ya mazingira, aliyekita katika kuwatetea wanawake, watoto, jamii za asili na makundi yenye mazingira hatarishi.
Taarifa ya kuteuliwa kwake imetolewa rasmi wiki hii Desemba 4,2025 na Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Kupambana na Uharibifu wa Ardhi na Ukame (UNCCD).
Mbali na kuwa Mwenyekiti wa JET, Dkt. Otaru pia ameshika nyadhifa mbalimbali za uongozi nchini Tanzania akiwa na uzoefu mpana katika usimamizi na tathmini ya miradi kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wa kimataifa pamoja na vyombo vya habari, ikiwemo Ubalozi wa Sweden (SIDA), Save the Children, UN Women na BBC Media.
RGDRP ni mpango mahususi (flagship initiative) wa UNCCD ambao pia unajumuisha Mfuko Maalum wa Utekelezaji ujulikanao kama Global Mechanism (GM).
0 Comments