Ticker

7/recent/ticker-posts

WATAALAMU WAPITIA MPANGO WENYE KUANGALIA NA KUTATHMINI NAMNA KUHIMILI MABADILIKO YA TABIANCHI

  

Jopo la wataalamu wakiwa Katika picha ya pamoja

NA JIMMY KIANGO-ARUSHA

Wataalamu kutoka sekta mbalimbali nchini wamekutana jijini Arusha Mei 16-17,2024 kwenye Hoteli ya New Arusha ili kupitia na kuthibitisha ripoti ya mapitio ya Sera, Sheria na Mipango ya Wizara za Kisekta kwa ajili ya kuangalia na kutathmini namna masuala kuhimili mabadiliko ya tabia nchi kwenye kila sekta.

Akifungua mkutano huo Kaimu Mkurugenzi-idara ya Mazingira, Deogratius Paul, aliwashukuru wataalamu kwa kutenga muda weo na  kujumuika katika mkutano huo muhimu wa Kuthibitisha Ripoti ya Mapitio ya Sera, Sheria, Mikakati na Mipango mbalimbali ya Wizara za kisekta kwa ajili ya kuangalia na kutathmini namna masuala ya uhimili wa mabadiliko ya tabianchi yamezingatiwa. 

Aidha alilishukuru  Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP chini ya ufadhili wa Mfuko wa Dunia wa Mabadiliko ya Tabianchi (GCF)  kwa kuwezesha kufanyika Mkutano huo kupitia Mradi wa Kujenga Uwezo wa Utayari wa Nchi Kuhimili Athari za Mabadiliko ya Tabianchi (NAP)

 


Paul alisema lengo kuu la mkutano huo  ni Kupitia na Kuthibitisha Ripoti ya Mapitio ya Sera, Sheria, Mikakati na Mipango mbalimbali ya Wizara za kisekta kwa ajili ya kuangalia na kutathmini namna masuala ya uhimili wa mabadiliko ya tabianchi yamezingatiwa. 

Mkutano huu ni muhimu sana katika kuhakikisha kwamba mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya tabinachi  yanazingatia maoni, michango na ushirikishwaji wa  wadau mbalimbali wa sekta za serikali na zisizo za kiserikali. 

 “Aidha,  Mapitio ya maandiko haya yatatuwezesha kutambua mapungufu yanayohitaji kufanyiwa kazi pamoja na kutoa michango yetu ya kitaalamu katika kuboresha ripoti hizo.”

Alisema Mabadiliko ya Tabianchi ni tatizo kubwa linaloikabili Tanzania hivi sasa.  


Sekta mbalimbali za kiuchumi, kijamii na kimazingira ikiwemo Kilimo, Ufugaji, Uvuvi, Utalii, Maji, Misitu, Miundombinu zimekuwa zikiathirika kwa kiasi kikubwa. 

“Moja ya njia muhimu tunayoweza kutatua changamoto hizi za Athari za Mabadiliko ya Tabianchi ni kupitia sera na mifumo ya kisheria  kwa ajili ya kutathmini ufanisi wa zana hizo, kuhuhisha “mainstreaming”, kusimamia na kuimarisha upangaji wa masuala ya uhimili wa mabadiliko ya tabianchi. 


“Hivyo, kikao hiki cha siku mbili ni muhimu sana katika kusaidia  kuimarisha mipango ya usimamizi wa masuala ya mabadiliko ya tabianchi  na maenedelo ya taifa kwa ujumla.

 

 

 

 

Post a Comment

0 Comments