Ticker

7/recent/ticker-posts

USAID,JET WAENDESHA MDAHALO WA KUTAFUTA NAMNA BORA YA JAMII KUSHIRIKI ULINZI WA SHOROBA

Wawasilishaji wa mada za mdahalo huo, Afisa Wanyamapori Mkuu na  Mratibu wa Mailasili, Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi, kutoka Ofisi ya Rais Tamisemi Hawa Mwechaga (mbele Kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Fortunata Msofe (mbele kulia).


NA JIMMY KIANGO
Maisha ya wanyamapori yana mchango mkubwa katika uendelevu wa mazingira na maisha ya binadamu kwa ujumla wake. Kwa lugha nyepesi unaweza kusema kuwa maisha ya Binadamu na wanyamapori hasa kwenye kutunza mazingira yanategemeana.

 

Hata hivyo kumekuwa na migongano baina ya Binadamu na Wanyama unaosababisha chuki na uadui kati ya pande hizo mbili hali inayosababishwa kwa kiasi kikubwa na uharibifu wa maeneo ya asili ya wanyama.

 

Uharibifu huo unawafanya wanyama kuingia kwenye hatari ya kuuawa ama kuzuriwa kutokana na kuonekana kuwa ni wavamizi wa maeneo ya binadamu.

Ukweli wa hilo umelisukuma Shirika la Misaada la Marekani (USAID) kupitia mradi wa USAID Tuhufadhi Maliasili kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET) kuendesha mradi wenye lengo la kupunguza kama si kuondoa kabisa changamoto hizo kwa kuzifufua na kuzilinda shoroba nchini bila kuathiri shughuli za binadamu.

 

Mradi wa USAID Tuhifadhi Maliasili andio umebeba dhamana hiyo ambao pamoja na mambo mengine umejielekeza kwenye kuleta tija kwa pande zote mbili.

Ikumbukwe kuwa ogezeko la watu na shughuli za kibinadamu ndizo zinatajwa kuwa kichocheo kikuu cha kuyaharibu mapito ya wanyama (ushoroba) nchini. 

Baadhi ya Waandishi wa Mazingira walioshiriki mdahalo huo.
Ushoroba ambayo ni mapito ya wanyamapori   huwasaidia kuhama kutoka hifadhi moja kwenda nyingine kutafuta malisho na maji. Hata hivyo kumekuwa na migongano baina ya binadamu na wanyamapori ambapo jamii zinazopakana na hifadhi zimekuwa zikifanya shughuli zao za kibinadamu katika maeneo hayo hali inayofikia kuyaharibu mapito hayo ya wanyama.

Ili kutafuta suluhu USAID na JET, Mei 14,2024 waliendesha mdahalo uliofanyika katika ofisi za Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Mikocheni, jijini Dar es Salaam ukishirikisha Waandishi wa Habari za Mazingira na wizara ya Maliasili na Utalii na Ofisi ya Rais Tamisemi.

Mdahalo huo ulilenga pia kutoa elimu kwa jamii kuchukua hatua za kuhifadhi shoroba kwa kutumia njia mbalimbali ili kuepukana na migongano baina yao na wanyamapori hasa tembo.Afisa Wanyamapori Mkuu na Mratibu wa Maliasili, Mazingira na mabadiliko ya Tabia nchi, Hawa Mwechaga alisema tembo ni fursa na kuna haja ya wananchi kuelimishwa juu ya hilo ili kuwa na utayari wa kuzilinda shoroba kwa tija.

“Wananchi wanapaswa kujua kuwa tembo ni fursa, tembo hapaswi kuwa adui, tunapaswa kuwaeleza wananchi juu ya suala hili, wakilielewa hili ni rahisi kwao kushiriki ulinzi wa shoroba,” alisema.

Akiifafanua kauli yake ya kuwa tembo ni fursa na si tatizo, alisema endapo wananchi watashiriki kulinda shoroba pamoja na kutofanya shughuli zao kwenye maeneo ya karibu na wanyamapori hao ni wazi wanyamapori hao hawataingia kwenye maeneo ya makazi ya watu, lakini pia itakuwa rahisi kwa wananchi kuendesha shughuli za utalii na kujiingizia kipato.

Mkurugenzi wa JET, John Chikomo aliyekaa kwenye kochi jeusi pamoja na Waandishi wa Havari za Mazingira wakifuatilia mjadala huo.

 Alisema yapo maeneo tayari wameichangamkia fursa hiyo na sasa wanajiingizia kipato, ambapo moja ya maeneo hayo ni vijiji nane vya wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi ambavyo vimekuwa vikipata kiasi cha shilingi bilioni 14 ikiwa ni gawio la miezi sita tu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Wanyamapori wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Fortunata Msofe, alisema wizara imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha shoroba zinalindwa.

 

Mkurugenzi wa JET, John Chikomo alisema chama hicho kitaendelea kushirikiana na wadau wa Mazingira ili kuhakikisha shoroba zinalindwa, lakini pia mazingira yanakuwa salama ili kuepukana na mafuriko na majanga mengine yanayochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Mwenyekiti wa JET, Dkt. Ellen Otaru (Kushoto) kushoto akiwa na Mkurugenzi wa JET, John Chikomo.


Post a Comment

0 Comments