Makamu wa Rais wa Namibia, Nangolo Mbumba sasa atakalia kiti cha urais wa nchi hiyo hadi pale Uchaguzi Mkuu utakapofanyika Novemba mwaka huu.Hatua hiyo ni kwa mujibu wa Katiba ya Namibia, inayooelekeza kuwa endapo Rais atafariki dunia au kupoteza uwezo wa kutekeleza majukumu yake basi Makamu wa Rais atakuwa Rais wa mpito hadi pale nchi itakapofanya uchaguzi.
Mbumba anachukua nafasi hiyo kufuatia kifo cha Rais Dkt. Hage Geingob (82) kilichotokea asubuhi ya leo Februari 4, 2024.
0 Comments