Rais Samia Suluhu Hassan amezipokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kilo cha kifo cha Rais wa Namibia, Hage Geingob kilichotokea asubuhi ya leo, Februari 4,2024, jijini Windhoek. Katika salamu zake za rambirambi alizozitoa kwa Taifa la Namia kupitia chanel yake ya WhatsApp, Rais Samia amesema Hayati Rais Geingob alikuwa rafiki mkubwa wa Tanzania.
"Nimehuzunishwa sana na kifo cha Rais wa Namibia, Mheshimiwa Hage Geingob, ndugu mpendwa, mwana Pan Africanist na rafiki mkubwa wa Tanzania.
"Kwa niaba ya wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, natuma salamu za rambirambi kwa wananchi wa Jamhuri ya Namibia, Kaimu Rais, Mheshimiwa Dkt. Nangolo Mbumba, Mke wa Rais, Mheshimiwa Monica Kalondo, familia, marafiki na wandugu. katika SWAPO.
"Ninyi nyote mfarijike katika kipindi hiki kigumu. Roho yake ipumzike kwa amani. Amina."
0 Comments