Ticker

7/recent/ticker-posts

KUHARIBIWA KWA MAENEO ASILI KUNA ATHARI KWA DUNIA

NA JIMMY KIANGO-AFRINWSSWAHILI- DSM 

Tunahitaji kuilinda vyema asili kwa maslahi yetu wenyewe, bila hatua kubwa za kuzuia kupotea kwa Bioanuwai msingi wa asili wa maisha ya binadamu utapotea kwa kasi isiyokuwa ya kawaida na kupatikana kwa madhara ya muda mrefu kwenye maeneo yote ya maisha. 

 Asilimia 50 ya uzalishaji wa uchumi wa dunia unategemea moja kwa moja asili. Katibu Mtendaji wa CBD Mrema alipata kusema kuwa tunategemea mazingira asili katika kuishi, lakini tunakuwa wa kwanza kuyaharibu.  

"Tunaharibu asili ingawa mapato yetu, chakula chetu, afya zetu na hewa tunayovuta vinaitegemea." Ikumbukwe kuwa Watalii wengi huvutiwa kuzitembelea nchi za Afrika ya Mashariki kutokana na urithi wa mbuga zake zenye wanyama wa kila aina. 

 Lakini kwa siku za karibuni, uwindaji haramu wa wanyama hao umekuwa ukiongezeka na sasa serikali zinahofia kupoteza mapato ya utalii na pia kuhatarishwa kwa mfumo wa uhusiano wa kimaumbile kati ya wanyama, wanaadamu na mimea.

Post a Comment

0 Comments