Ticker

7/recent/ticker-posts

DRC YAKUMBWA NA MAPOROMOKO YA UDONGO

Watu 15 wametajwa kufariki dunia katika maporomoko ya udongo katika vitongoji viwili vya Bukavu, jiji kubwa lililopo mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 

Hii ni kwa mujibu wa shirika la habari la AFP likinukuu vyanzo vya ndani na mashahidi. 

Kwenye mji mkuu wa Kivu Kusini, ambako Rais Félix Tshisekedi alifanya mkutano wa kampeni siku ya Ijumaa wiki iliyopita kuelekea uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Desemba 20,2023 mvua kubwa ilisababisha maporomoko hayo ya udongo na kusomba nyumba kadhaa.

Wilayani Ndendere, baba, watoto wake watano na wajukuu wawili walifukiwa na udongo na nyumba yao kuharibiwa kabisa, kutokana na maporomoko hayo yaliyotokea usiku.

Nayo wilaya maarufu iliyojirani na Panzi ambayo imejengwa hospitali ya mshindi wa Tuzo ya Nobel na daktari wa magonjwa ya wanawake Denis Mukwege, watu saba wameripotiwa kufariki dunia katika mazingira kama hayo.

Post a Comment

0 Comments