Ticker

7/recent/ticker-posts

WAZIRI UMMY AWAONYA WAMILIKI WA MADUKA YA DAWA NA WAFAMASIA


​Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa onyo kali kwa wafamasi na wamiliki wa maduka ya dawa waotoa dawa bila kuangalia cheti cha daktari kwa kuwa kufanya hivyo ni kuendeleza tatizo la usugu wa vimelea vya magonjwa dhidi ya dawa na kuhatarisha afya za watu.

Waziri Ummy amesema hayo jana Novemba 17, 2023 wakati akifunga Kongamano la Tatu la Usugu wa Vimelea dhidi ya Dawa na kufungua rasmi wiki ya uhamasishaji na uelimishaji jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa inayoanza leo Novemba 18 hadi 24, 2023.

“Nataka wafamasia wote nchini kuacha mara moja tabia ya kutoa dawa ikiwemo za Antibiotiki bila cheti cha daktari na nikimkamata mtu siku moja nitampiga faini kubwa kama sio kumfungia duka kabisa.” Amesema Waziri Ummy.


Amesema, atatuma timu kufanya kaguzi za kushtukiza kwenye maduka ya dawa, ambapo amesisitiza mfamasia atakaebainika kutoa dawa za Antibiotiki bila cheti cha daktari atafikishwa mahakamani na atalipa faini kubwa.

Aidha, Waziri Ummy amewataka wataalamu wa Afya kuzingatia Mwongozo wa Taifa wa Matibabu wanapo wahudumia wagonjwa ili  kufanikisha kampeni ya ‘Afya Moja’ yenye lengo la mapambano ya Usugu wa Vimelea vya Magonjwa dhidi ya Dawa.

Post a Comment

0 Comments