Ticker

7/recent/ticker-posts

AUCHO AWEKWA NJE MICHEZO MITATU

Bodi ya ligi kuu Tanzania bara imemfungia michezo mitatu mchezaji wa klabu ya Yanga, Khalid Aucho pamoja na kutozwa faini ya Sh laki tano kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union Ibrahim Ajibu katika mechi iliyochezwa Uwanja wa Mkwakwani Tanga Novemba 8 mwaka huu.

Taarifa ya bodi ya ligi iliyotolewa  leo Novemba 17 , 2023 imeeleza kuwa adhabu hiyo kwa kuzingatia kanuni 17 kifungu cha 60 ya ligi kuu kuhusu taratibu za michezo.

Aidha,Klabu ya Coastal Union imetozwa faini ya Sh milioni moja kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka kwenye chumba cha kubadilishia nguo, Jambo lililosababisha mchezo huo kuchelewa kuanza kipindi cha kwanza na baada ya mapumziko.

Pia,Mwamuzi katika mechi hiyo Emmanuel Mwandembwa kutoka Arusha amefungiwa kwa miezi sita (6) kwa kufanya kazi ya uamuzi wa mpira miguu,kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu jambo ambalo limesababisha ashindwe kumudu mchezo huo.

Katika hatua nyingine Klabu za Simba na Yanga zimetozwa faini ambapo Yanga imetozwa faini ya Sh milioni 5 kwa kutumia mlango usio rasmi kwenye mchezo dhidi ya Simba huku Simba wakitozwa faini ya Sh milioni  moja kwa wachezaji wake kuchelewa kutoka kwenye vyumba vya kubadilishia nguo kwenye mchezo dhidi ya Yanga uliopigwa Novemba 5, 2023 Uwanja wa Benjamini Mkapa.

Post a Comment

0 Comments