Mtu aliyetoa ushauri wa kujengwa kwa karakana ya mabasi ya mwendo wa haraka kujengwa Jangwani, jijini Dar es Salaam ametakiwa kuwaomba radhi Watanzaia.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa.
Mchengerwa amesema mshauri huyo amewakosea sana Watanzania.
Ameyasema hayo katika ziara yake kwa Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) na kudai kuwa karakana hiyo imejengwa bila kuzingatia baadhi ya sheria za Baraza la Mazingira (NEMC) kwa kuwa eneo hilo kihalisia ni mkondo wa maji
“Kwa kweli aliyeshauri karakana ile ijengwe pale Jangwani amewakosea sana Watanzania, eneo lile halifai na limeiletea serikali hasara kubwa, fedha nyingi zimetumika kujenga pale na sasa hivi inabidi karakana ihamishwe na pale pabomolewe, hasara tupu.
“Mfano sasa hivi mnataka kuhamisha Depo kwenda sehemu nyingine mnapoweka mipango yenu mjue eneo hilo lipo salama kusiwe na changamoto kama Jangwani,”amesema Mchengerwa.
Eneo la Jangwani ilipo Karakana hiyo imekuwa ikipigiwa kelele muda mrefu na wadau wa mazingira kuwa ujenzi wake haukuzingiatia tathmini iliyofanywa na NEMC wala haukuzingatia sheria za mazingira.
0 Comments