Taarifa iliyochapishwa na gazeti la The New York Times la nchini Marekani, linaeleza kuwa Urusi inatafuta silaha zaidi kwa ajili ya vita vyake nchini Ukraine, na wajumbe wa Korea Kaskazini hivi majuzi walisafiri hadi Urusi kwa treni kupanga ziara ya Kim.
Rais wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un anapanga kusafiri hadi Urusi mwezi huu kukutana na Rais Vladimir Putin kujadili uwezekano wa kuipatia Urusi silaha zaidi kwa ajili ya vita vyake vya Ukraine na ushirikiano mwingine wa kijeshi.
Katika msafara wa nadra Kim atasafiri kutoka Pyongyang, mji mkuu wa Korea Kaskazini, pengine kwa treni ya kivita, hadi Vladivostok, kwenye Pwani ya Pasifiki ya Urusi, ambako atakutana na Putin, wamesema Maafisa wa Marekani.
Putin anataka Kim akubali kutuma makombora ya kivita ya Urusi na makombora ya kuzuia vifaru, na Kim angependa Urusi iipe Korea Kaskazini teknolojia ya hali ya juu ya satelaiti na nyambizi zinazotumia nyuklia, maafisa hao walisema, Kim pia anatafuta msaada wa chakula kwa taifa lake maskini.
Viongozi wote wawili watakuwa kwenye kampasi ya Chuo Kikuu cha Shirikisho la Mashariki ya Mbali huko Vladivostok ili kuhudhuria Kongamano la Kiuchumi la Mashariki, ambalo limepangwa kuanza Septemba 10 hadi 13, kulingana na maafisa. Kim pia anapanga kutembelea Pier 33, ambapo meli za wanamaji kutoka kituo cha meli cha Pasifiki cha Urusi, walisema. Korea Kaskazini inaadhimisha kumbukumbu ya kuanzishwa kwake Septemba 9.
Siku ya Jumatano, Ikulu ya White House ilionya kwamba Putin na Kim walikuwa wamebadilishana barua wakijadili uwezekano wa mpango wa silaha, wakinukuu taarifa za kijasusi zilizofichwa. Msemaji wa Ikulu ya White House, John F. Kirby, alisema mazungumzo ya ngazi ya juu kuhusu ushirikiano wa kijeshi kati ya mataifa hayo mawili "yanaendelea kikamilifu."
Marekani ilikataa kutoa maelezo zaidi kuhusu hali ya uhusiano wa binafsi wa viongozi hao, ambao wanachukuliwa kuwa wapinzani wa Marekani.
0 Comments