Ticker

7/recent/ticker-posts

BEI YA MAFUTA YA PETROL YAPANDA ZAIDI

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza kupanda kwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini zitakazotumika kuanzia leo Jumatano Septemba 06, 2023 saa 6:01 usiku ambapo kwa mwezi Septemba 2023, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam ilikuwa ni petrol ni Tsh. 3213 kwa lita, dizeli Tsh. 3259 na mafuta ya taa 2943.

EWURA imesema mabadiliko ya bei za mafuta kwa mwezi Septemba 2023 yaliyoonesha kupanda kwa bei yanatokana na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia kwa asilimia 21, gharama za uagizaji wa mafuta hadi 62% ikilinganishwa na mwezi August 2023 na maamuzi ya kisiasa katika nchi zinazozalisha mafuta kwa wingi (OPEC+).

Itakumbukwa kuwa bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini kwa mwezi uliopita zilizoanza kutumika kuanzia Jumatano Agosti 02, 2023 saa 6:01, bei za rejareja za mafuta katika Mkoa wa Dar es Salaam petrol ilikuwa ni Tsh. 3199 kwa lita, dizeli Tsh. 2935 na mafuta ya taa 2668.

Post a Comment

0 Comments