Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Citizens Coalition for Change (CCC), kimemtuhumu rais wa nchi hiyo, Emmerson Mnangagwa kwa “upendeleo” kwa ndugu zake baada ya kuwateua mtoto wake, David Kudakwashe na binamu yake Tongai Mnangagwa katika safu mpya ya baraza la mawaziri baada ya kuchaguliwa tena kuiongoza Zimbabwe kwa muhula wa pili mwishoni mwa mwezi uliopita.
Moja ya vyombo vya habari vya nchi hiyo kimetangaza kuwa David Kudakwashe amechaguliwa kuwa naibu waziri wa fedha na Tongai Mnangagwa amechaguliwa kuwa naibu waziri wa utalii.
Baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakieleza kutoridhishwa na uteuzi huo wa baraza la mawaziri.
Chanzo BBC
0 Comments