Ticker

7/recent/ticker-posts

MCHUNGAJI KIMARO ATOA TAHADHARI KWA NDUGU KUSAFIRI PAMOJA


​Mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Kijitonyama, Dar es Salaam Mch. Eliona Kimaro ametoa wito kwa wasafiri kuepuka ndugu au wanafamilia kutumia usafiri wa pamoja ili kuepusha wimbi la vilio na simanzi kwa familia na ndugu wa pamoja pale inapotokea ajali au tukio lingine lisilozuilika

Amesema hayo wakati akiongoza ibada ya kuaga mwili wa Nechi Msuya aliyefariki kwenye ajali ya gari mkoani Pwani walipokuwa safarini kuelekea mkoani Kilimanjaro kuzika mmoja wa ndugu yao akiwa ameambatana sambamba na dada zake watatu huku Nechi akiwa dereva wa gari hiyo

Katika ibada hiyo iliyofanyika kwenye Kanisa la KKKT Kijitonyama, Mchungaji Kimaro amesema ni ngumu na ni siri iliyofichwa na Mungu kuhusu ajali, kifo na mengineyo lakini ipo haja ya kutafakari na kujiuliza kama familia na wanandugu wanasafirije kwa maana ya kuchukua tahadhari inayostahiki kwa mwanadamu.

Baada ya ibada hiyo, mwili wa Nechi umesafirishwa kuelekea Ugweno, Kilimanjaro ambako atapumzishwa kwenye makazi yake ya milele jana Jumapili Agosti 06.2023, wakati dada zake wakitarajiwa kuzikwa Jumanne, Agosti 08.2023, katika makaburi ya Kondo, yaliyopo Ununio, jijini Dar es Salaam.


Post a Comment

0 Comments