Tamasha la klabu ya Simba, limefana kwa kiwango cha kimataifa ambapo Rais Samia Suluhu Hassan amelinogesha zaidi.
Jana Rais Samia aliwaongoza mashabiki wa Simba katika kilele cha tamasha hilo na kurejea ahadi yake ya kununua kila goli kwa klabu za Tanzania zinazoshiriki mashindano ya Kimataifa.
Rais Samia Suluhu Hassan ameongeza kuwa Tanzania inaendelea na maandalizi ya kuwa mwenyeji wa Mashindano ya AFCON kwa kushirikiana na nchi jirabni za Kenya na Uganda kwa kujenga viwanja vipya viwili vya kisasa katika mikoa ya Arusha na Dodoma.
Katik tamasha hilo, Simba ilijipima ubavu na timu ya Power Dynamos ya Zambia, ambapo iliibuka na ushindi wa bao 2-0 ambazo wafungaji wake ni wachezaji wao wapya.
0 Comments