Madaktari bingwa 60 wa mifupa na nyongo kutoka California nchini Marekani wanatarajia kuwasili Tanzania kesho Agosti 10, 2023 kwa ajili ya kutoa huduma ya matibabu bure ya upasuaji wa magoti na nyonga katika Hospital ya Rufaa ya Seliani inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT).
Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Arusha, Kaimu Mkurugenzi wa Hospital ya Seliani, Dkt. Godwin Kivuyo amesema madaktari hao watawasili nchini saa 2 usiku katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Kilimanjaro (KIA) na watafanya shughuli za upasuaji kwa wagonjwa 200 muda wa wiki mbili.
Dkt. Kivuyo amesema mbali na huduma hiyo ya upasuaji pia watakuwa wakitoa mafuzo kwa madaktari bingwa wa hospital hiyo katika kuhusu shughuli za upasuaji.
Alisema kuwa wagonjwa watakaopata huduma ya upasuaji wa magoti na nyonga kwa madaktari hao ni wale tu wenye uwezo wa hali ya chini kwani ndio walengwa.
"Ujio wa madaktari bingwa wa mifupa kutoka nchini Marekani ni fursa kwa Hospitali ya Seliani na pia ni neema kwa Watanzania wenye kukabiliwa na magonjwa hayo.amesema Kivuyo.
0 Comments