Janga la Covid 19, vita barani ulaya na mabadiliko ya tabianchi vimeipa somo serikali na inajipanga vizuri kuhakikisha inakuwa na akiba ya chakula cha kutosha.
Hayo yamesemwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Rais Samia ameyasema hayo leo June 13, 2023 jijini Mwanza alipokuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Utamaduni la Bulabo linaloendelea katika Uwanja wa Red Cross Ngomeni Kisesa jijini humo.
Amesema, kutokana na sababu hizo tatu hatua stahiki tayari zimeshachukuliwa za kuongeza matumizi katika sekta ya kilimo ili watu wavune zaidi na Taifa kuwa na akiba ya kutosha ya chakula.
Rais amesisitiza kuwa serikali ina mpango wa kusajili wakulima ili iwatambue ni watu wangapi wanajishughulisha na sekta hiyo ili ijipange vizuri.
0 Comments