Hatua ya Serikali ya Korea kuendelea kuiunga mkono Tanzania, umemfanya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dk.Hussein Ali Mwinyi kutoa shukurani kwa nchi hiyo.
Serikali ya Korea imekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwenye masuala mbalimbali ya maendeleo hasa sekta ya uchumi wa buluu.
Dk.Mwinyi ametoa shukurani hizo Ikulu, Zanzibar leo alipozungumza na Mkuu wa Taasisi ya bahari ya Korea, Dk.Kim Jong-Deog aliyefika kwa mazungumzo pamoja na kumualika katika Kongamano kubwa la Afrika Mashariki litakakalojadili fursa na rasilimali za bahari zitakazoakisi azma ya zana nzima ya uchumi wa buluu nchini.
Dkt. Mwinyi alisema anaamini mkutano huo utawajengea uwezo wananchi wengi zaidi katika kujikomboa na kujifunza mengi yatakayotokana na mkutano huo na kueleza kuwa ni fursa nzuri kwa ustawi wa sekta ya uvuvi Zanzibar.
0 Comments