Ticker

7/recent/ticker-posts

WAFUNGWA THAILAND KUANZA KULIPWA

BUNGE la nchini Thailand limepitisha muswada wa sheria utakaowezesha wafungwa kuanza rasmi kulipwa kuanzia mwaka huu mpya wa fedha.

Chini ya muswada huo mpya  utaoundiwa kanuni baada ya kuwa sheria,umefafanua kuwa wafungwa watalipwa kulingana ukubwa wa vifungo na aina ya makosa pamoja na kuzingatia umri.

Muswada huo ukipitishwa kuwa sheria utasaidia sana kupunguza adha za kiuchumi zinazowakabili wafungwa wa vifungo virefu na wale ambao hawana ndugu wa kuwaletea mahitaji maalum ya kibinadam wa kiwa gerezani.

Baadhi ya Wabunge wamepongeza hatua hiyo ya serikali huku wakisisitiza kuwa utaratibu wa malipo hayo usimamiwe vizuri ili fedha hizo zisiende kwa wasiohusika.


Awali akiwasilisha muswada huo Bungeni mwanasheria mkuu wa serikali ya Thailand Wootikon Mamason alisema sheria hiyo mpya pia itaweka kanuni za kipengele cha bima ya afya ambapo hela zitakatwa kupitia malipo hayo na hivyo kufanya Thailand kuwa nchi ya kwanza kulipa wafungwa na pia kuwapa bima ya matibabu.

Post a Comment

0 Comments