Matokeo ya 2-1 iliyoyapta Yanga kwenye mchezo wake wa kusaka tiketi ya kwenda fainali ni wazi yamepandisha thamani ya kocha wake Nasridin Nabi na mshambuliaji wake hatari, Fiston Mayele.
Yanga sasa imefanikiwa kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kufanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu ya Marumo Gallants uliochezwa Afrika Kusini.
Ikumbukwe kuwa kweye mchezo wa mkondo wa kwanza uliochezwa Tanzaia, Yanga ilipata ushindi wa mabao 2-0.
Leo Yanga ilianza kupata bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Fiston Kalala Mayele akipokea pasi nzuri kutoka kwa Kennedy Musonda na kuzamisha moja kwa moja wavuni..
Kipindi cha pili Yanga iliendelea kulisakama lango la mpinzani kwa kutengeneza nafasi nyingi ambazo walishindwa kuzitumia ingawa jitihada za Mayele zilisaidia na kuweza kupata bao la pili kupitia kwa Musonda, goli lililotengenezwa na Fiston Mayele.
Ushindi huo unaifanya Yanga kuweka historia ya kutinga ya micbuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Yanga imetangulia fainali kwa jumla ya Mabao 4-1 na sasa wanaisubiri USM Alger au ASEC Mimosas ambao wanacheza baadae leo.
0 Comments