Ticker

7/recent/ticker-posts

RAIS RUTO AIFUMUA IDARA YA USALAMA WA TAIFA KENYA

AfrinewsSwahili, Nairobi 

Rais William Ruto, amemteua Haji Noor kuwa Mkurugenzi Mkuu mpya wa idara ya Usalama wa Taifa, ya nchi hiyo.

Haji Noor ameelezwa kurudi kundini kuchukua nafasi ya Meja Jenerali, Philip Wachira Kameru ambaye amestaafu.

Katika waraka wa Serikali kwa umma uliosainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi wa nchi hiyo Felix K. Koskei, Rais Ruto amemsifu Mkurugenzi Mkuu aliyemaliza muda wake. Kwa utumishi mzuri na wa kukumbukwa aliouonesha tangu alipoteuliwa kushika nlwadhifa huo mwaka 2014.

Kabla ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa, Meja Jenerali Wachira Kameru alikuwa Mkuu wa Kitengo cha Usalama Jeshini ( Military Intelligence) cha Jeshi la Ulinzi la Nchi hiyo.

Rais Ruto ameelezea utumishi wa Meja Jenerali Kameru kama alama inayobaki katika historia ya nchi hiyo kwa namna alivyowajibika kizalendo na kitaalamu katika kuzuia ugaidi, uhalifu wa kimataifa na matishio mbali mbali dhidi ya Usalama wa nchi hiyo na ukanda  wa Afrika Mashariki.

Waraka wa Katibu Mkuu Kiongozi  Felix Koskei ukieleza wasifu wa Mkurugenzi Mkuu mpya Haji Noor, umefahamisha kwamba, kabla ya uteuzi mpya, Mbobezi huyo alikuwa Mkurugenzi wa Mashtaka ya jinai nafasi aliyoihudumu kwa miaka sita na kabla ya hapo alikuwa Naibu Mkurugenzi wa Kitengo cha uzuiaji uhalifu wa kupanga cha Idara ya usalama wa Taifa.

Noor Haji ana shahada ya kwanza ya sheria, kadhalika shahada ya umahiri ya Sheria kutoka Chuo Kikuu cha Wales Cardiff nchini Uingereza na pia ana shahada ya umahiri katika masuala ya utunzi wa Sera juu ya Usalama wa Taifa.

Aidha mwaka 1999 hadi 2000 alifanya kazi kama Mwanasheria katika ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali akiwa pia afisa wa idara ya Usalama.

Post a Comment

0 Comments