Msaidizi wa Rais wa Uganda, Yoweri Museven kwenye masuala ya Kazi, Ajira na Uhusiano wa Viwanda Nchini humo, Charles Okello Engola ameuawa asubuhi hii kwa kupigwa risasi na Mlinzi wake (Bodyguard).
Rais Museven alimkabidhi Okello kiti cha uwaziri wa masuala ya Kazi,Ajira na uhusiano wa viwanda.
Spika wa Bunge la Uganda Anitha Among amethibitisha kutokea kwa tukio hilo bungeni leo.
Tukio hilo limetokea asubuhi ya leo, imeripotiwa kuwa Waziri Okello alikuwa anatoka nyumbani kwake kwenda kazini ambapo ghafla mlinzi wake alimpiga risasi kisha akaanza kupiga risasi juu huku akikimbiakimbia mtaani.
Hayati Okello enzi za uhai wake
Majirani wamesema Mlinzi huyo alisikika akisema hajalipwa mshahara kwa muda mrefu licha ya kufanya kazi yake kwa moyo na akili yake yote.
Mlinzi huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo aliingia Saluni moja iliyopo jirani na nyumba ya Waziri kisha akawataka waliokuwa ndani kutoka nje na akajifungia na kujipiga risasi na kufariki pia.
0 Comments