Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imeomba Bunge iidhinishie kiasi cha shilingi trilioni 3,554,783,957,000.00.
Fedha hizo zimegawanywa katika maeneo mawili, eneo la Ujenzi na eneo la Uchukuzi.
Maombi hayo yametolewa na Waziri wa Wizara hiyo, Prof Makame Mbarawa bubgeni leo jijini Dodoma.
Waziri Mbarawa amewasilisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2023/24 ya wizara yake.
Alisema kati ya fedha hizo, shilingi 1,468,238,449,000.00 ni Kwa ajili ya sekta ya Ujenzi na shilingi 2,086,545,508,000.00 ni Kwa ajili ya sekta ya Ujenzi.
Kwenye mwaka wa fedha wa 2022/23 sekta ya Ujenzi ilitengewa jumla ya shilingi 44,293,050,000.00 kwa ajili ya matumizi ya kawaida. Kati ya fedha hizo shilingi 40,638,652,00.00 ni kwa ajili ya mishahara ya watumishi wa Wizara na Taasisi zake.
Shilingi 3,654,398,000.00 zilikuwa ni matumizi ya kawaida ya wizara na taasisi zake.
0 Comments