Nchi waasisi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Tanzania, Kenya na Uganda wameomba kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) za mwaka 2027.
Nchi hizo zinaingia kwenye orodha ya nchi sita zilizoomba kuandaa fainali hizo zikiwa pamoja na Algeria, Botswana na Misri.
Nchi hizo tatu zenyewe kila moja zimeomba kuandaa binafsi tofauti na nchi hizo za Afrika Mashariki.
Maombi ya nchi hizo yatapitiwa na CAF, Juni 1-15 mwaka na kutolewa uamuzi.
0 Comments