Bondia chipukizi wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Ibrahim Najum kutoka jijini Mbeya amefariki dunia mchana wa leo katika Hosptali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma ( General) alipokuwa akipatiwa matibabu.
Najum alianguka ulingoni jumapili iliyopita baada tu ya kumalizika kwa pambano lake la raundi nne dhidi ya Bondia wa Dodoma Laurent Segu, na kuwahishwa Hosptali ambapo inaarifiwa alifanyiwa upasuaji mdogo wa kichwa hadi asubuhi ya leo hali yake ilizidi kuimarika kabla ya kufikwa na umauti mchana wa leo.
Bondia huyo alikuwa amecheza mapambano matatu tu ya ngumi za kulipwa pamoja na hilo pambano la Jumapili iliyopita, ambapo ameshinda moja na kupoteza mawili.
Mwili wa Ibrahim Najum ambaye inadaiwa kabla ya kupanda alingoni alipigwa na kitu kizito na mkewe tayari umeanza safari kuelekea Kyela Mbeya kwa ajili ya mazishi.
0 Comments