Ukitaka kujua kwanini hili sakata la Hakimi limegusa hisia za wapenda soka wengi kutoka Afrika, soma hii stori ya Emmanuel Eboue utaelewa kitu.
Emmanuel Eboue raia wa Ivory Coast stori yake ni yenye kuhudhunisha licha ya kuwa inawazonga wanasoka wengi hasa wa Afrika wakistaafu ama kufkia kikomo kimichezo.
"Talaka kati ya Eboue na mkewe aliyetambulika kwa jina la Aurellie ilimfanya Eboue kuwa na msongo wa mawazo mkubwa uliochangiwa na kuzuiliwa kuwatembelea kabisa watoto wake watatu Mathis, Clara na Maeva.
Kosa lilianzia pale Eboue alipompa mkewe mamlaka na haki ya kumiliki mali zote walizokuwa nazo na kitendo cha kutalakiana kinamaanisha Eboue alipoteza kila kitu alichomuandikishia mwanamke huyo baada ya kushindwa kesi ya talaka mahakamani.
Inasemekana kuwa alisaini makaratasi ya kumkabidhi mali mwanamke bila kutambua kwasababu hakuwa na elimu ya kutosha ukijumlisha na mahaba ya kijambazi, mwamba akamwaga wino.
Wakati Eboue anaachana na mke wake alikuwa ametoka kufiwa na babu yake nchini Ivory Coast aliyefariki kwa kansa huku kaka yake aliyefahamika kwa jina la N’Dri Serge naye alifariki kwa ajali ya pikipiki.
Matatizo ya Eboue ya umiliki wa baadhi ya vitu ikiwemo nyumba yake ya kisasa iliyokuwa London na hakuwa na pesa ya kuwalipa wanasheria hali ambayo ilipelekea baadhi ya nyumba na mali alizobakiwa nazo kuuzwa.
Mbaya zaidi Eboue aliwahi kukiri kuwa na mawazo ya kujiua kutokana na hali ilivyobadilika katika maisha yake na alikuwa akimuomba Mungu sana amuondolee mawazo hayo mabaya kichwani mwake.
Baada ya hapo Eboue alianza maisha mapya katika nyumba ya rafiki yake ambapo inasemekana alikuwa akilala chini huku hana hata pesa ya kupelekea nguo dry cleaner hali iliyomfanya kutumia mikono yake kufua nguo.
0 Comments