Ticker

7/recent/ticker-posts

NDIZI ZAADIMIKA KWENYE BAADHI YA MAENEO BUKOBA

Kupanda kwa gharama za maisha, ukame na changamoto ya mnyauko wa migomba kumetajwa kuwa sababu kubwa ya kuadimika kwa zao la ndizi kwenye maeneo mengi mkoani Kagera.

Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kamachumu, wilayani Muleba ambako kunatajwa kuwa kitovu cha ndizi mkoani humo, hali kweli ni mbaya.

Kijiji hicho ambacho kipo umbali wa kilomita 50 kutoka Bukoba mjini, kwa sasa kinakabiliwa na uhaba wa ndizi, hali iliyowasababishia na wao wenyewe kuhamishia mlo wao wa siku kwenye ugali.

Kankiza Bashaija, anasema wamelazimika kuhamia kwenye ugali kwa sababu ya kuadimika kwa ndizi.


"Ndizi zimekuwa adimu, ukipata mkungu mmoja uliokomaa unashukuru Mungu angalau utakula na watoto au utauza ili ununue unga.

Akizungumzia sababu ya kupanda kwa bei ya ndizi Bukoba mjini, mfanyabiashara aliyejitambulisha kwa jina la Ishengoma, alisema hali hiyo imesababishwa na kuongezeka kwa bei za bidhaa nyingi, ukame na ugonjwa wa mnyauko kwenye migomba.

"Bidhaa nyingi zimepanda Bei, sio rahisi ndizi ikabaki kwenye Bei hiyo hiyo, lakini pia kuna ugonjwa wa mnyauko pamoja na ukame.

"Hatujawahi kuuza ndizi tano kwa shilingi 1000, lakini sasa tunauza hivyo, hali si nzuri."

Post a Comment

0 Comments