Ticker

7/recent/ticker-posts

​SIMBA YAINGIZA MILIONI 410.6 YAAMBULIA MILIONI 188.9

Timu ya Simba ambayo ndio ilikuwa mwenyeji wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Yanga, imejikuta ikapata mgao wa shilingi milioni 188,987,181.10 kutoka kwenye kiasi cha shilingi milioni 410,645,000 zilizopatikana kwenye mchezo huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jumla ya watazamaji walioingia uwanjani kushuhudia mchezo huo ni 53,569.

Kati ya mashabiki hao, 340 walilipa kiingilio cha VIP A kwa kiingilio cha shilingi 30,000 na kupatikana jumla ya sh.10,200,000.

VIP B walioingia watazamaji 4,160 kwa kiingilio cha sh. 20,000 na kiasi cha sh.83,200,000 kilipatikana.

VIP C walioingia watazamaji 2004 kwa kiingilio cha sh.15,000 na kupatikana sh. 30,060,000, jukwaa la rangi ya Machungwa walioingia watazamaji 10,372 Kwa kiingilio cha sh. 10,000 na kiasi cha sh.103,720,000 na jukwaa la mzunguko walioingia watazamaji 36,693 kwa kiingilio cha sh.5,000 na kupatikana jumla ya sh.183,465,000.

Kiasi hicho cha fedha kiligawanywa katika maeneo tisa ambayo ni VAT sh. 62,640,762.71, BMT sh.10,440,127,12, gharama za tiketi sh. 22,585,475 na uwanja ni sh.47, 246,795.28


Maeneo mengine yaliyopata mgawo huo ni gharama za mchezo sh.22,048,504,46, TFF sh.12,599,145.41, TPBL sh. 25,198,290.81, FA mkoa sh. 18,898,718.11 na kiasi kilichosalia kilikwenda kwa timu ya Simba.

Katika mchezo huo wa watani wa jadi uliochezwa Jumapili Aprili 16, mwaka juu Simba ilishinda bao 2-0.

Post a Comment

0 Comments