Marehemu Hussein Jumbe wakati wa uhai wake
Taarifa zilizotufikia jioni hii zimebainisha kuwa mwanamuziki Hussein Jumbe amefariki dunia Alasiri ya leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana, jijini Dar es Salaam, alikokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa Meneja wake, Jumbe alikuwa anasumbuliwa na vidonda vya tumbo.
Meneja wake Heri Shaban amezungumza hayo kupitia TBC 2 na msiba wake na taratibu zote zitafanyika Tuangoma.
0 Comments