Aishi Manula
Nyota wetu wawili mlinzi wa kati, Henock Inonga na mlinda mlango, Aishi Manula walipata maumivu katika mchezo wetu wa Robo Fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Ihefu uliopigwa juzi Uwanja wa Azam Complex.
Wachezaji hao walishindwa kuendelea na mchezo huo ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 5-1 na kutupeleka nusu fainali ya michuano ya ASFC.
Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema nyota hao jana wamepelekwa hospitali na wamefanyiwa vipimo ili kujua ukubwa wa majeraha waliyopata.
Dk. Edwin amesema Inonga hajapata majeraha makubwa amepewa mapumziko ya siku mbili na ataungana na kikosi baada ya kurejea kutoka jijini Mbeya.
Kwa upande wa Manula yeye atafanyiwa vipimo zaidi Jumanne ingawa inaonekana hajapata majeraha makubwa.
0 Comments