MALIPO YA BIMA YAMUWEKA PABAYA

 

Hatua ya kulipa bima kwa muda mrefu bila kupata majanga imemsukuma mfanyabiashara mkoani Njombe kujikuta matatani baada ya kudaiwa kuchoma maduka likiwemo lake ili bima imlipe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Njombe, Hamis Issah ameweka wazi kuwa mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kutekeleza tukio hilo Aprili mosi mwaka huu kwenye milango inayomilikiwa na Jumuiya ya Wanawake wa CCM (UWT) wilaya ya Njombe.

Kabla ya kufanya kitendo hicho inadaiwa alihamisha bidhaa zake huku akiamini baada ya kuchoma moto atalipwa fidia ya bidhaa zilizokuwamo dukani kwake.

 

 

Post a Comment

0 Comments