Ticker

7/recent/ticker-posts

FOUNTAIN GATE YAING'ARISHA TANZANIA KWENYE SOKA

Ushindi walioupata Fountain Gate Dodoma Secondary School dhidi ya Ecole Omar IBN Khatibu ya Morocco wa bao 3-0 kwenye mchezo  wa fainali ya African Schools Championship hii leo, umewapa ubingwa Fountain na Tanzania kwa ujumla.

Mabao ya Fountain yamefungwa na Winfrida Hubert (2), na Irene Chitanda , baada ya ushindi huo, Fountain wamepata Dola 300,000 ambazo ni sawa na Shilingi Million 630.

Ushindi huo umeipa Fountain gate kuvuna Million 860, ambapo pia walifanikiwa kuwa mabingwa wa ukanda wa CECAFA na kupata kiasi cha sh. Million 230.

Post a Comment

0 Comments