Ticker

7/recent/ticker-posts

ALLY ASHINDWA KUHIMILI YA DUNIANI, AJINYONGA

Ally Hamis (48) ameshindwa kuhimili vishindo vya duniani na kuamua kujiua ili kuepuka msururu wa madeni uliomuandama.

Mwanaume huyo amefikia hatua hiyo juzi akiwa chumbani kwake  katika kijiji cha Itwangi Wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga.

Ili kuhakikisha kifo chake hakiachi madhila Kwa wengine, Ally aliandika  ujumbe uliobeba Sababu za uamuzi wake huo.

Sababu ya msingi ni madeni yaliyomuandama na aliwaomba Ndugu zake wambebee mzigo huo wa madeni. 

Ni ndugu zake ndio walio kuwa wa kwanza kuugundua mwili wa Ally ukiwa umening'inia.

Mwenyekiti wa kijiji cha Itwangi, Kisendi Lubinza yeye  amesema Ally ameacha ujumbe kwa kuorodhesha madeni anayodaiwa na kuwaomba ndugu zake kuyalipa.

Baadhi ya madeni yaliyoachwa na Ally  ni la  baskeli yake aliyokuwa anadaiwa sh 40,000/= , baba yake mdogo anamdai laki tatu na mwingine alipwe debe moja la mahindi.

"Kwenye ujumbe wake pia ameandika  ‘nimeamua kujiua mimi mwenyewe asishikiliwe mtu yoyote nimeamua kwa moyo wangu, nimeamua kumfuata mama yangu aliyetangulia mbele za haki miaka mingi iliyopita", ameeleza Mwenyekiti huyo wa kijiji.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

“Ni kweli mwanaume huyo amejinyonga na ameacha ujumbe kuwa ana madeni.

Post a Comment

0 Comments