Ticker

7/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU ATAKA KITUO CHA MABASI BARIADI KIANZE KUTUMIKA

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameagiza stendi kuu ya mabasi katika mji wa Bariadi mkoani Simiyu ianze kutumika kwa mabasi makubwa na madogo ili kuondoa usumbufu kwa abiria.

"Mkuu wa Mkoa wekeni utaratibu utakaofaa ili mabasi yaanzie pale na kuishia pale lakini haimaanishi kuwa muwapitilize abiria wanaoshukia au kupandia njiani.”

Ametoa agizo hilo leo asubuhi (Jumapili, Machi 26, 2023) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Mji wa Bariadi katika eneo la stendi ya zamani akiwa njiani kuelekea Maswa.


"Jana nilitembelea pale stendi kuu na kuona fedha za Serikali zinapotea bure. Kuna vibanda 148 vya wajasiriamali lakini hawafanyi kazi kwa sababu hakuna abiria wanaoingia na kutoka. Kuna vijana wa bajaj na bodaboda wamejipanga vizuri lakini hawana kazi kwa sababu hakuna mabasi,” amesema.

Amesema Serikali ilitoa sh. bilioni 7 ili zitumike kuupanga mji wa Bariadi na pia ikaanzisha mfumo wa anuani za makazi ili uwepo urahisi wa kufikika. “Lazima tujipange vizuri ili mji huu upangike. Huu mji ni makao makuu ya mkoa, kwa hiyo malori hayatakiwi kupaki holela hapa mjini bali yaende kwenye eneo lake lililotengwa.”


Post a Comment

0 Comments